MALTA-ITALIA-PAPA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji kwenye Pwani ya Malta: Papa atoa wito kwa viongozi wa EU kuwa na ushirikiano

Papa Francis katika Kanisa kuu ya Mtakatifu Petro katika mji wa Roma, Januari 1, 2019.
Papa Francis katika Kanisa kuu ya Mtakatifu Petro katika mji wa Roma, Januari 1, 2019. REUTERS/Tony Gentile

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametoa wito kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuonesha mshikamo ili kuwasaidia wahamiaji 47 waliokwama ndani ya meli za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Pwani mwa Malta.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Malta na Italia zimekataa kuwapokea wahamiaji hao, ambao kwa siku kadhaa sasa wamesalia ndani ya meli hizo.

Papa Francis amewaomba viongozi wa Ulaya kuelewa uhai wa wahamiaji hao na kuwaruhusu kuingia katika mataifa hayo.

Licha ya wito huo ambao pia umetolewa na Tume ya Umoja wa ulaya, serikali ya Malta na Italia zimeonekana kutokuwa tayari kufungua milango yao kwa wahamiaji hao.