UFARANSA-USALAMA

Vizibao vya njano: Serikali ya Ufaransa yatangaza hatua kali dhidi ya wahalifu

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe katika mahojiano na TF1, Januari 7, 2019.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe katika mahojiano na TF1, Januari 7, 2019. ERIC FEFERBERG / POOL / AF

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe ametangaza hatua kali dhidi ya wahalifu wanaojificha katika maandamano yanayoendelea nchini humo kwa kuzua machafuko.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na TF1, Edouard Philippe amesema wale wote wanaoandaa maandamano bila kibali watapewa adhabu.

Onyo hili limekuja, baada ya kushuhudiwa kwa wiki saba za waandamano katika miji mbalimbali nchini humo siku za Jumamosi, kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.

Aidha, Waziri Mkuu wa Ufaransa anataka bunge kupitisha mswada utakaopiga marufuku watu wanaonekana kuwa wagomvi kushiriki kwenye maandamano lakini wasivalie mavazi au kofia za kufunika uso wakati wa maandamano.

Maandamano hayo ya kila Jumamosi, yamekuwa yakishuhudia makabiliano makali kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.