UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Theresa May ajikuta kwenye wakati wakati mgumu

Theresa May amezuru ngome ya wafuasi wa wanaotaka Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ualaya huko Stoke-on-Trent, Januari 14, 2019.
Theresa May amezuru ngome ya wafuasi wa wanaotaka Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ualaya huko Stoke-on-Trent, Januari 14, 2019. Ben Birchall/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, amekuwa katika harakati za lala salama, kuwashawishi wabunge kuunga mkono mkataba uliofikiwa kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya, kuhusu namna nchi hiyo itakavyokuwa baada ya kujiondoa kwenye umoja huo mwezi Machi.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wanatarajiwa kupigia kura mswada huo siku ya Jumanne wiki hii huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda wakaukataa.

May amesema iwapo, wabunge wataukataa mkataba huo, itamaanisha kuwa wanataka nchi hiyo isalia kwenye Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya, wamesema hawewezi kuja tena katika meza ya mazungmzo kujadili upya mkataba huo.