UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Theresa May kuwasilisha "Mpango B" mbele ya bunge

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May. REUTERS/Hannah McKay

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anatarajia kuwasilisha mpango wa pili "mpango B" leo Jumatatu alasiri, Januari 21, mbele ya Bunge la nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya unabaini kwamba uamuzi kwa sasa uko upande wa Theresa May na wabunge kukubaliana juu ya kupinga mapendekezo ya mkataba wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya ulifikiwa kati ya Waziri Mkuu wa Uingereza na umoja huo ambao ulipingwa.

Umoja wa Ulaya unasema wajumbe wake katika mazungumzo hayo watarejea mezani kama makubaliano hayo yatakuwa yamefikiwa.

Baada ya kushindwa katika mpango wake wa kwanza (mpango A), Theresa May anatarajia kuwashawishi wabunge kabla ya kuwasilisha mpango wake wa pili mbele ya bunge la Uingereza.

Kukataliwa kwa mpango huo ni pigo kubwa kwa Theresa May na serikali yake.

Uamuzi wa wabunge umekaribishwa na wafuasi wanaotaka kupigwa kura mpya ya maoni.

Hivi karibuni wanasiasa mbalimbali walitoa wito wa kufanyika kwa kura mpya ya maoni ili kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea.

Hata hivyo serikali ya Theresa May ilifutilia mbali hoja hiyo, ikisema itazidisha mgawanyiko na kukiuka uamuzi wa wananchi wa Uingereza ambao walipiga kura Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2016.

Muda wa mwisho Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya utakamilika Machi 29, 2019 siku.