UGIRIKI-MAKEDONIA-SIASA

Bunge la Ugiriki laidhinisha jina jipya la Makedonia

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras na Waziri Mkuu wa Makedonia Zoran Zaev kabla ya kusaini mkataba tata wa muda mrefu kuhusu jina la zamani la Yugoslavia katika kijiji cha Psarades, huko Prespes, Ugiriki, Juni 17, 2018.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras na Waziri Mkuu wa Makedonia Zoran Zaev kabla ya kusaini mkataba tata wa muda mrefu kuhusu jina la zamani la Yugoslavia katika kijiji cha Psarades, huko Prespes, Ugiriki, Juni 17, 2018. 路透社。

Hatimaye Makedonia imebadilishwa jina na kuwa Jamhuri ya Makedonia ya Kaskazini. Jina hilo jipya limefikiwa baada ya bunge la Ugiriki kudhinisha makubaliano kuhusu jina hilo kati ya Athens na Skopje mnamo mwezi Juni mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Makedonia tayari imeidhinisha mabadiliko haya ya jina. Waziri Mkuu Zoran Zaev amekaribisha hatua ya bunge la Ugiriki kusahihisha makubaliano hayo.

Hatua hizi mbili za kuidhinisha makubaliano hayo zitaruhusu kuondoa kura za veto zilizopigwa na Athens katika miaka ya hivi karibuni kwa kuiunganisha katika siku za baadae Makedonia kwa Umoja wanchi za kujihami za Magharibi (NATO) na Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, ameweza kupata wabunge wengi bungeni ili kuidhinisha makubaliano na Skopje, kwa msaada wa baadhi ya Wabunge waliowania kwa viti vyao binafsina wabunge kutoka upinzani.