UFARANSA-BENALLA-HAKI-USALAMA

Kesi ya Benalla: Mkuu wa usalama Matignon ajiuzulu, rafiki yake asimamishwa kazi

Kesi ya mahojiano yaliyo rekodiwa kati ya Alexandre Benalla na Vincent Crase imezua hali nyingine ya sintofahamu nchini Ufaransa. Mkuu wa usalama wa Waziri Mkuu Edouard Philippe (Matignon) amejiuzulu kwenye nafasi yake tangu Alhamisi jioni.

Mkuu wa usalama wa waziri mkuu, ambaye aliingia matatani kutokana na uhusiano wake na Alexandre Benalla, aamua kujiuzulu Alhamisi.
Mkuu wa usalama wa waziri mkuu, ambaye aliingia matatani kutokana na uhusiano wake na Alexandre Benalla, aamua kujiuzulu Alhamisi. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kujiuzulu kwa Marie-Elodie Poitout inakuja saa 48 baada ya kusikilizwa na maafisa wa uchunguzi Jumanne wiki hii. Wakati huo Marie-Elodie Poitout alieleza kwamba hahusiki na kile anachoshtumiwa.

Marie-Elodie Poitout amesema ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake ili "kuepusha utata wowote". kwamba mkuu wa usalama wa Waziri Mkuu alisema.

Katika mahojiano na Edouard Philippe, alieleza kwamba hajawahi kupanga mkutano wowote kati ya Alexandre Benalla na Vincent Crase, ambao wote wawili wako chini ya sheria za mahakama tangu mwishoni mwa mwezi Julai. Mkutano uliopigwa marufuku, na ambao hata hivyo ulifanyika, kulingana na sauti zilizorikodiwa.

Lakini Marie-Elodie Poitout alielezea maafisa wa uchunguzi Jumanne wiki hii kuwa hahusiki na mkanda huo wa sauti ulifichuliwa na Mediapart.

Katika mkanda huo Alexandre Benalla na Vincent Crase wanasikika wakijivunia kupata uungwaji mkono kutoka kwa rais Emmanuel Macron, wakati huo huo serikali imekuwa ikitangaza kwamba imejitenga na watu wawili.

Afisa wa jeshi, Chokri Wakrim, ambaye ni rafiki wa Marie-Elodie Poitout alisimamishwa kazi tangu Jumatano wiki hii kwa mujibu wa vyombo vya habari, baada ya kushiriki katika mkataba uliofikiwa kati ya Alexandre Benalla na tajiri mmoja wa urusi.

Hatma ya Chokri Wakrim itajulikana hadi pale mwanga utatolewa kuhusu madai hayo," kwa mujibu wa AFP.