UJERUMANI-ULAYA-SYRIA-IS-USALAMA

Berlin: Ni vigumu wanajihadi kutoka Ulaya kurejea nyumbani

Heiko Maas, hapa, ilikuwa Mei 9, 2018: kuhusu kurejea kwa wanajihadi kutoka Ulaya nyumbani, "tunahitaji habari za mahakama, na hali hii bado haijafikiwa".
Heiko Maas, hapa, ilikuwa Mei 9, 2018: kuhusu kurejea kwa wanajihadi kutoka Ulaya nyumbani, "tunahitaji habari za mahakama, na hali hii bado haijafikiwa". Odd ANDERSEN / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump amezitaka nchi za Ulaya kuwarejesha nyumbani wanamgambo wa kigeni wa kundi la Islamic State (IS) waliokamatwa nchini Syria. Wito huo umeibua mjadala katika nchi kadhaa za Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa marekani amzitaka Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pamoja na nchi nyingine za Ulaya kuchukua zaidi ya wapiganaji 800 wa IS, ambao wamekamatwa na Marekani na wawafungulie mashtaka "vyenginevyo atalazimika kuwaachilia huru."

Ujerumani inasema kuwarejesha nyumbani watu hao na watoto wao pamoja na wake zao itawazekana iwapo watafunguliwa washtaka na kukamatwa pale tu wanapowasili nchini. Lakini Maas amesema kama hilo halitowezekana basi itakuwa vigumu kuwarejesha nyumbani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema sharti hilo la Trump litakuwa "vigumu sana kutekelezwa."

Serikali za nchi za Ulaya zimekuwa na wasiwasi, kuhusu kuwarudisha nyumbani raia wao waliokwenda kuwaunga mkono IS kwa kupigana nchini Syria na Iraq. Wanahofia athari za kisiasa, zitakazotokana na kuwarejesha nyumbani watu makatili hasa kufuatia mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya kigaidi nchini Ufaransa, Ujerumani na kwengineko Ulaya.