UFARANSA-BENALLA-HAKI-USALAMA

Mshauri wa zamani wa Emmanuel Macron awekwa chini ya ulinzi

Alexandre Benalla, mbele ya Kamati ya Uchunguzi ya Bunge la Seneti, Paris, Septemba 19, 2018.
Alexandre Benalla, mbele ya Kamati ya Uchunguzi ya Bunge la Seneti, Paris, Septemba 19, 2018. REUTERS/Charles Platiau

Alexandre Benalla anatarajia kufikishwa jela, baada ya jaji kuamua Jumanne wiki hii kuwa hakuheshimu utaratibu wa sheria aliopewa, katika uchunguzi wa ghasia za tarehe 1 Mei 2018 mjini Paris.

Matangazo ya kibiashara

Alexandre Benalla, mshauri wa zamani wa rais Ufaransa Emmanuela Macron alitakiwa kuripoti yeye na rafiki yake Vincent Crase, katika mahakama ya Paris Jumanne asubuhi.

Januari 31, Mediapart ilitoa mazungumzo ya siri yaliyorekodiwa kati ya wawili hao, tarehe 26 Julai, siku nne baada ya kufunguliwa mashitaka, wakati mahakama iliwakataza kuwasiliana.

Kufuatia hoja ya mwendesha mashtaka, majaji wanaoendesha kesi hiyo waliomba mamlaka husika (JLD) na kuamuru Alexandre Benalla kuwekwa chini ya ulinzi. Kesi ya Vincent Craseilitarajiwa kujadiliwa Jumanne jioni.

Hata hivyo mwanasheria wa Alexandre Benalla, wakili Jacqueline Laffont amesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo, ili mteja wake aachiliwe huru.