IRAQ-UFARANSA-USHIRIKIANO

Rais wa Iraq Barham Saleh azuru Ufaransa

Rais wa Iraq Barham Saleh, Baghdad Januari 30, 2019.
Rais wa Iraq Barham Saleh, Baghdad Januari 30, 2019. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Rais wa Iraq Barham Saleh anaanza Jumatatu hii, Februari 25 ziara ya siku mbili nchini Ufaransa. Rais wa Iraq na mwenyeji wake Emmanuel Macron, wanatarajia kuzungumzia kuhusu ushirikiano wa usalama na biashara, lakini pia kuzungumzia kuhusu hatima ya wanajiahdi wa Ufaransa wanaoendelea kuwepo katika kanda hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ingawa wanamgambo wa kundi la Islamic State hawadhibiti tena maeneo ya Iraq, Ufaransa itaendelea kusalia nchini Iraq kwa kutoa mafunzo, kutoa msaada wa vifaa vya jeshi na kupeana taarifa.

Hatima ya wanajihadi wa Ufaransa itakuwa miongoni mwa masuala yatagubika mazungumzo kati ya Emmanuel Macron na Barham Saleh. Paris inataka raia wake wanaozuiliwa nchini Iraq wahukumiwe nchini humo.

Vyanzo kadhaa vinabaini kwamba wanajihadi wa kigeni wakiwemo raia wa Ufaransa waliokamatwa nchini Syria walihamishwa hivi karubuni nchini Iraq. Ikiwa taarifa hii itathibitishwa, wanajihadi hao watafikishwa katika mahakama za Iraq na hivyo kupunguza uwezekano wa kuwatuma katika nchi zao za Ulaya, ambapo suala hili limezua mjadala mkubwa.

Suala la ujenzi wa Iraq na kubadilishana kiuchumi pia litakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo kati ya Emmanuel Macron na Barham Saleh.