Pata taarifa kuu
UHISOPANIA-UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Brexit: Waingereza 400,000 kupewa makaazi Uhispania

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alibaini  mbelea ya wabunge Jumanne (Februari 12) kwamba "anahitaji muda" wa kujadili na EU mabadiliko ya makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya yaliyofikiwa na Brussels.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alibaini mbelea ya wabunge Jumanne (Februari 12) kwamba "anahitaji muda" wa kujadili na EU mabadiliko ya makubaliano ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya yaliyofikiwa na Brussels. Getty Images/Volker Schlichting / EyeEm
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Uhispania iinapanga kuwapa makaazi raia 400,000 kutoka Uingereza kama Uingereza itajiondoka katika Umoja wa Ulaya bila makubaliano, limeripoti gazeti la El Pais, siku moja baada ya serikali ya Uhispania kuchapisha hatua ambazo inapanga kuchukuwa.

Matangazo ya kibiashara

Ili hatua hii itumike, hata hivyo, Madrid itahitaji usawa kwa wananchi wa Uhispania wanaoishi na kufanya kazi nchini Uingereza, gazeti la Al Pais limeongeza.

Kipaumbele cha Uhispania ni kwamba hakuna raia wa Uhispaniola au Uingereza atakadhulumiwa haki zake baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Waziri wa Mambo ya Nje Josep Borrell amewambia waandishi wa habari baada ya kuhojiwa leo Ijumaa na gazeti la El Pais.

Mpango wa dharura wa Uhispania pia unahusu kesi la Gibraltar, gazeti hilo limeandika, ingawa Madrid itahitaji kuwa na kauli kuhusu hatua yoyote kuhusiana na rasi hiyo.

Rasimu ya sheria inayojumuisha hatua za mpango wa dharura itawasilishwa haraka kwa Bunge, kabla ya kufutwa kwa minajali ya uchaguzi wa haraka wabunge mwishoni mwa mwezi Aprili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.