New Zealand: Arobaini wauawa katika mashambulizi dhidi ya miskiti miwili Christchurch
Imechapishwa:
Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya watu wane kufanya mashambulizi katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema.
Maofisa wa polisi wametumwa katikati mwa jiji la Christchurch baada ya mashambulizi ya risasi katika misikiti miwili nchini New Zealand. Polisi, ambayo inasema "watu wengi wameuawa, imewakamata watu kadhaa.
Kwa mujibu wa chanzo cha polisi katika eneo la tukio, vizuizi vimeanza kuondolewa kwenye barabara za mji huo mara baada ya polisi kutangaza kuwa wamekamata watu wanne na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.
1/6 Police continue to respond to an ongoing serious and tragic firearms incident in Christchurch.The incident remains fluid and information is still coming to hand.We can confirm that Police have been dealing with two shootings at two mosques in Christchurch...
New Zealand Police (@nzpolice) March 15, 2019
"Watu wane, wanamume watatu na mwanamke mmoja, wanashikiliwa na polisi, " amesema, mkuu wa polisi katika eneo hilo Mike Bush, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huku akibiani kwamba jeshi lilitegua kilipuzi kilichopatikana katika magari ya watuhumiwa.
Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.
Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".
Awali mkuu wa pilisi katika mji wa Christchurch amesema watu waliouawa ni wengi, lakini hakutaja idadi.