UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Uingereza kuamua ikiwa inataka kuepuka Brexit bila mkataba

Waziri Mkuu Theresa May akiondoka Downing Street Aprili 3, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Waziri Mkuu Theresa May akiondoka Downing Street Aprili 3, 2019 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Peter Nicholls

Viongozi wa Ulaya wanatarajia kujadili Jumatano Aprili 9 kuhusu kuahirishwa tena kwa tarehe ya mwisho ya mchakato wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Uingereza inatakiwa kuelezea mpango wake wa kuepuka kujiondoa katika umoja huo bila mkataba, Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ujerumani amesema leo Jumanne.

"Kwa bahati mbaya, nitazungumza kwamba mazingira yaliyowekwa na Baraza la Ulaya katika mkutano wake wa mwisho hayakuwa mazuri. Kwa hiyo ninamaanisha kwamba muda wa mwisho ni tarehe 12 Aprili," Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ujerumani, Michael Roth, amewaambia waandishi wa habari alipofika Luxembourg, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni unaoanda mkutano wa Jumatano jijini Brussels.

"Kwa sasa tunasubiri hatua za msingi katika mwelekeo sahihi. Hadi sasa hakuna chochote kilichobadilika. Tunafikiria kuongeza muda unaofaa wa tarehe ya mwisho na pia kusogeza mbele kwa muda mrefu, "amesema Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ujerumani.

"Tuko katika hali mbaya, na Umoja wa Ulaya unapaswa kutatua matatizo yake ya baadaye. Tunapaswa kuipa muda Uingereza kufafanua kile wanachotaka," ameongeza.

"Inaonekana, mazungumzo na upinzani wa Uingereza, ambayo yalianza baada ya kuchelewa, hayakuzaa matunda yoyote."

Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Romania, George Ciamba, kwa upande wake amesema kuwa Uingereza inapaswa kuelezea viongozi wa Umoja wa Ulaya jinsi itakavyotumia muda inaotaka, ambao utakuwa umeongezwa.

Romania kwa sasa ndio mwenyekiti wa wa Umoja wa Ulaya.