Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAJANGA ASILI

Ufaransa: Moto uliozuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame wadhibitiwa

Jumanne hii asubuhi, kikosi cha Zima Moto cha Paris kinaendelea kuzima moto ulizuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame.
Jumanne hii asubuhi, kikosi cha Zima Moto cha Paris kinaendelea kuzima moto ulizuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame. Zakaria ABDELKAFI / AFP

Kikosi cha wazima moto zaidi ya 400 jijini Paris wamefaulu kuudhibiti moto ulivamia majengo ya kanisa kongwe la Notre-Dame, mfumo mzima wa jengo umeokolewa lakini paa lote zimeharibiwa na moto. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kujenga upya mnara huo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuki na paa zima la Kanisa la Notre-Dame, ambalo ni mfano wa mji mkuu wa Ufaransa, ulianguka jioni ya Jumatatu, Aprili 15, kutokana na moto. Hata hivyo moto huo ulidhibitiwa usiku baada ya masaa kadhaa.

Afisaa mmoja wa kikosi cha zima moto amethibitisha kuwa nguzo na muundo wote mzima wa jengo umeokolewa huku mmoja miongoni mwa wazima moto akijeruhiwa vibaya.

Rais wa Ufaransa Emmauel Macron aliahirisha hotuba yake kwa taifa na kuelekea kwenye eneo la tukio ambapo ameahidi kuwa kanisa hilo litajengwa huku akipongeza kuona maeneo muhimu yameokolewa.

Uchunguzi kuhusu kubaini chanzo cha moto huo umeamzishwa na mahakama jijini Paris. Wafanyakazi waliokuwa katika ujenzi uliokuwa ukiendelea katika kanisa hilo tayari wamehojiwa na polisi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.