Pata taarifa kuu
UFARANSA-DINI-MAJANGA ASILI

Macron: Tutalijenga upya Kanisa Kuu la Notre-Dame 'ndani ya kipindi cha miaka mitano'

Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kutoka Elysée, Jumanne, Aprili 16.
Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kutoka Elysée, Jumanne, Aprili 16. © Élysée

Saa 24 baada ya kutokea kwa moto mkali ulioteketeza sehemu ya jengo la Kanisa Kuu kongwe la Notre-Dame jijini Paris, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa hotuba yake fupi kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron amependekeza Jumanne wiki hii kuwa ujenzi wa Kanisa Kuu la Notre-Dame de Paris litakamilika katika kipindi cha miaka mitano na ni nafasi kwa Ufaransa kuungana tena katika mradi wa pamoja.

Rais huyo wa Ufaransa amesema wakati wa hotuba yake hiyo kwamba atatangaza katika siku zijazo hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na mgogoro wa waandamanaji wenye vizibao vya njano, lakini wakati haujafika.

Emmanuel Macron alilazimika kuahirisha hotuba yake siku ya Jumatatu jioni kutokana na moto huo ulioteketeza sehemu ya jengo la Kanisa Kuu la Notre-Dame de Paris. Hata hivyo hakuweka wazi ni lini atatangaza hatua alizozichukuwa kusaka suluhu ya mzozo wa waandamanaji wenye vizibao vya njano.

Sikiliza hotuba ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.