UFARANSA-KAZI-USALAMA

Usalama waimarishwa katika miji mbalimbali Ufaransa

Waandamanaji wakishiriki katika maandamano ya "vizibao vya njano" ya kila Jumamosi", Paris, Aprili 27, 2019
Waandamanaji wakishiriki katika maandamano ya "vizibao vya njano" ya kila Jumamosi", Paris, Aprili 27, 2019 Zakaria ABDELKAFI / AFP

Polisi jijini Paris hii leo wanajiandaa kukabiliana na mamia ya waandamanaji waliopanga kujitokeza kwenye viunga vya miji mbalimbali nchini humo kuadhimisha siku ya Wafanyakazi na kupinga sera za rais Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita waandaaji wa vizibao vya njano waliitisha maandamano makubwa hivi leo, maandamano ambayo Serikali imesema haitakuwa na huruma na waandamanaji ambao watashiriki kufanya vurugu.

Mashirikisho ya wafanyakazi nchini Ufaransa pia yamewataka raia kujitokeza kwa wingi hii leo kushinikiza kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na maslahi.

Ufaransa imeendelea kukabiliwa na maandamano ya vizibao vya njano kila Jumamosi ya wiki.