EU-THERESA MAY-UINGEREZA

May: Mswada wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya kuwekwa wazi mwezi Juni

Waziri Mkuu wa Uingereza  Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May REUTERS/Toby Melville/File Photo

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema mswada wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, hautajadiliwa au kuchapishwa hadi mapema mwezi Juni.

Matangazo ya kibiashara

May ametoa kauli hii wakati huu anapoendelea kupata shinikizo, ajiuzulu baada ya kuahidi kuwa ataleta mswada mpya.

Hii inakuja baada ya mmoja wa Waziri Andrea Leadsom, kujiuzulu Jumatano usiku kuhusu mpango mpya wa Waziri May.

Waziri Mkuu May, siku ya Jumatano, aliwaambia wabunge wana nafasi ya mwisho kuamua mustakabali wa nchi hiyo kujiondoa kwenye umoja huo au waamue kuwa na kura nyingine ya maoni.

Uingereza imepewa hadi mwisho wa mwezi Oktoba kupitisha mswada wa kujiondoa kwenye Umoja huo.