UINGEREZA-MAY-EU-SIASA

Waziri Mkuu Theresa May apata shinikizo za kujiuzulu

Theresa May Waziri Mkuu wa Uingereza
Theresa May Waziri Mkuu wa Uingereza Kirsty Wigglesworth/Pool via REUTERS

Waziri mkuu wa uingereza Bi .Theresa may ameendelea kukabiliwa na shinikizo kali kutoka kwa wabunge wa chama chake wakimtaka kujiuzulu baada ya moja kati ya Mawaziri wake wa juu kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa shughuli za bunge, Andrea Leadsom, kufuatia sera ya Brexit ya Waziri Mkuu May.

May amewaambia wabunge kuwa wana nafasi ya kipekee ya kuwapa wananchi wa taifa hilo uamuzi wa kujiondoa kwenye Umoja huo au la wanaweza kuamua, kufanyike kwa kura ya pili ya maoni.

Mawaziri wengine kadhaa wamenukuliwa wakisema kuwa Waziri Mkuu hawezi tena kubaki katika wadhifa huo, kauli ambayo imeungwa mkono na Jeremy Corbyn kiongozi wa upinzani kupitia chama cha Labour.

Uingereza imepewa na Umoja wa Ulaya had mwisho wa mwezi Oktoba kukubaliana kuhusu mkataba uliofikiwa kati ya nchi hiyo na vongozi wa Umoja wa Ulaya.

Wabunge kwa nyakati tatu tofauti, wamekataa mkataba wa Waziri Mkuu May wakimtaka afanye mazungumzo zaidi na wakuu wa EU.