UINGEREZA-MAY-EU-SIASA

Waziri Mkuu Theresa May huenda akatangaza ni lini atajiuzulu

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anatarajiwa kutangaza tarehe ya kujiuzulu kwake siku ya Ijumaa, chanzo kimoja kutoka bungeni kimeliambia Shrika la Habari la Uingereza BBC.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akizungumza bungeni may 22 2019
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akizungumza bungeni may 22 2019 REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Bunge linataraji Waziri Mkuu huyo kutaja ratiba ya mrithi wake kuchaguliwa, kuelekea tarehe 10 mwezi Juni ambapo  huenda ikawa tarehe rasmi ya kuanza mbio za uongozi.

Bi.May anatarajiwa kukutana  na  Mwenyekiti wa  chama chake  cha  Conservative kujadili juu  ya  hatma yake huku tayari kuna idadi  kadhaa  ya viongozi wa  chama  cha  Conservative  ambao wako  njiani kuwania  wadhifa  wa  Waziri Mkuu May.

May yumo katika  shinikizo kubwa  kutaja tarehe ambayo ataondoka  madarakani baada  ya juhudi zake za mwisho za mpango wa kujitoa  kutoka  Umoja  wa Ulaya, yaani  Brexit kushindwa,

Tangu mwezi Januari bunge lilikataa mkataba wa kujitoa kati ya Theresa May na EU kwa mara tatu na majaribio ya hivi karibuni kupata muafaka wa pamoja na chama cha Labour kushindwa.