UINGEREZA-THERESA-MAY-SIASA-EU

Theresa May ajiuzulu rasmi kama Waziri Mkuu wa Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza aliyejiuzulu Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza aliyejiuzulu Theresa May Kirsty Wigglesworth/Pool via REUTERS

Theresa May siku ya Ijumaa, anajiuzulu rasmi kama Waziri Mkuu wa Uingereza na chama chake cha Conservative.

Matangazo ya kibiashara

May aliamua kuachia madaraka miaka mitatu baada ya kuingia madarakani, na hii imekuja baada ya wabunge kukataa kuunga mkono mpango aliokubaliana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu hatima ya nchi hiyo, baada ya kujiondoa kwenye Umoja huo.

Hata hivyo May, atasalia Waziri Mkuu hadi pale mrithi wake atakapopatikana mwezi Julai.

Tayari wanasiasa 11 ndani ya chama cha Conservative, wameonesha nia ya kutaka kumrithi Bi. May.

May alikuwa Waziri Mkuu wa pili mwanamke nchini humo baada ya Margaret Thatcher.

Harakati zake kuongoza Uingereza nje ya Umoja wa Ulaya, zilikwama mara tatu baada ya wabunge kukataa kuunga mkono mapendekezo yake.

Kabla ya uteuzi huo, alihudumu kwa miaka sita kama Waziri wa Mambo ya ndani.