Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI

Amano: Iran imeanza kurutubisha nyuklia, Marekani yaonya

Mkurugenzi shirika la umoja wa mataifa la Atomic, Yukiya Amano.
Mkurugenzi shirika la umoja wa mataifa la Atomic, Yukiya Amano. REUTERS/Heinz-Peter Bade
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
Dakika 2

Shirika la umoja wa Mataifa linalosimamia matumizi ya nguvu za Atomic, linasema kuwa nchi ya Iran imeanza kurutubisha urani kwa kasi kuliko kawaida, matamshi inayotoa wakati huu mvutano kati ya Iran na Marekani ukishika kasi.

Matangazo ya kibiashara

Tathmini ya IAEA inakuja wakati huu Marekani na Iran zikiwa zinakinzana, mwaka mmoja tu baada ya utawala wa Washington kutangaza kujitoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kutangaza vikwazo vipya.

Marekani ilitangaza vikwazo zaidi mwezi Mei mwaka huu ikizitaka nchi na makampun mbalimbali duniani kuacha kuagiza mafuta kutoka Iran au zikabiliwe na vikwazo vya kifedha.

Utawala wa Washington pia ulituma wanajeshi zaidi kwenye eneo la mashariki ya kati kwa kile ilichosema wanajukumu la kukabiliana na kitisho vya Iran dhidi ya nchi washirika.

Nchi ya Iran iliamua kujibu hatua ya Marekani kwa kutishia kuanza tena urutubishaji wa Urani, ikisema hatma ya nchi hiyo iko mikononi mwa mataifa ya Ulaya ambayo ni wadhamini waliosalia wa makataba waliotiliana saini.

Mkurugenzi wa shirika la atomic. Yukia Amano, amesema kwa sasa Iran inarutubisha Urani kwa kiwango cha juu bila ya kuweka wazi ni lini itaweza kufikia kiwango cha juu cha kilo 300 zitakazohatarisha usalama wa dunia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.