MAREKANI-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Barua zilizovuja zazua uhasama kati ya Marekani na Uingereza

Rais wa Marekani Donald Trump, Juni 25, 2019.
Rais wa Marekani Donald Trump, Juni 25, 2019. MANDEL NGAN / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump amemshambulia Waziri Mkuu wa Uingereza anaye maliza muda wake, Theresa May, baada ya balozi wa Uingereza nchini Washington, Sir Kim Darrach kukashifu utawala wa Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Sir Kim anawakilisha malkia wa Uingereza na serikali ya Uingereza nchini marekani.

Katika barua pepe zilizofichuliwa siku ya Jumapili, Sir Kim aliutajaa utawala wa rais Trump kama usiofanya kazi na usiojielewa. Wakati huo huo Bi May alisema kuwa ana imani na Sir kim lakini hakubaliana naye kwa maneno hayo.

Baada ya kukasirishwa na hatua ya Theresa May kumuunga mkono balozi huyo, Rais trump alimshtumu Bi May na kuanza kusema vile alivyoshindwa kusimamia Brexit.

Rais Trump pia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akimshutumu waziri mkuu wa Uingereza Theresa May akisema kuwa ''ni habari njema kwamba Uingereza itapata waziri mkuu mpya''.

Bi May alijiuzulu baada ya kukosa kuungwa na bunge kuhusu mpango wake wa Brexit, na chama tawala kinachagua kati ya mgombea Boris Johnson au Jeremy Hunt, kuchukua nafasi yake.