UGIRIKI-USALAMA-MAJANGA ASILI

Ugiriki: Kimbunga chaua watalii sita na kujeruhi wengine kadhaa

Watalii sita kutoka nchi za kigeni, ikiwa ni pamoja na watoto wawili, wametoweka, na watu 30 wamejeruhiwa baada ya kimbunga kikubwa, kupiga eneo la Chalkidiki, kaskaini mwa Ugiriki usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii.

Wanawake wawili wakikagua taverns za tavern huko Nea Plagia, waliharibiwa siku moja kabla ya kimbunga kitokea Chalkidiki, kaskazini mwa Ugiriki.
Wanawake wawili wakikagua taverns za tavern huko Nea Plagia, waliharibiwa siku moja kabla ya kimbunga kitokea Chalkidiki, kaskazini mwa Ugiriki. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kwa muda wa dakika tano tu tulijikuta tumeingiliwa na balaa kubwa," Haris Lazaridis, mmiliki wa mgahawa wa Nea Plagia ameliambia shirika la Habari la AFP.

Radio ya taifa ya ERT imesema wakiwanukuu polisi na kikosi cha ulinzi wa umma kuwa wote waliofariki ni watalii. Eneo lililoathirika zaidi na hali hiyo mbaya ya hewa ni kisiwa kinachopendelewa zaidi na watalii cha Chalkidiki.

Katika mgahawa wa Nea Plagia, mtu mmoja mwenye umri wa miaka 54, kutoka Romania na mwanae mwenye umri wa miaka 8 wameangamia wakati paa la mgahawa huo lilipong'olewa na kimbunga hicho.

Migahawa na baa zilizo kando ya pwani zilikuwa zimejaa wakati huu ambapo ni mwanzo wa msimu wa majira ya joto na ghafla, hali hiyo ikatokea, huku watu wakiingiliwa na "hofu".

"Watu wengi wamepiga kelele au kukimbilia kujificha ndani, " ameongeza Haris Lazaridis, akisema kuwa watu zaidi ya mia moja walikuwa pale wakati myu huyo alipoangukiwa na paa iliyotengenezwa kwa mbao, wakati mvulana wake alisukumwa na upepo mkali kabla ya kuangukia kio cha dirisha.

Eneo hili maarufu kwa utalii, ambapo hali ya dharura ilitangazwa, lilionekana likikumbwa na hali mbaya ya hewa.