EU-UJERUMANi-SIASA

Hatima ya Ursula von der Leyen kujulikana Jumanne hii

Ursula von der Leyen anatakiwa kutoa ushawishi wa kutosha kwa wabunge 374 ili wampigie kura kwenye nafasi ya Mkuu wa Tume ya Ulaya.
Ursula von der Leyen anatakiwa kutoa ushawishi wa kutosha kwa wabunge 374 ili wampigie kura kwenye nafasi ya Mkuu wa Tume ya Ulaya. REUTERS/Francois Lenoir

Bunge la Ulaya linatarajia kuamua Jumanne hii Julai 16 kuhusu uteuzi wa Ursula von der Leyen kama Mkuu wa Tume ya Ulaya. Hata hivyo chama cha SPD kinaendelea kupinga uteuzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Chama cha SPD wamepinga uteuzi wa Ursula von der Leyen baada ya mgombea wao, Mholanzi Frans Timmermans, aliyeondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania uenyekiti wa Tume ya Ulaya.

Wiki iliyopita, wabunge kumi na sita wa chama cha SPD katika Bunge la Ulaya ambao walikataa kumpigia kura mwananchi mwenzao walikuwa wamewapa wenzao kutoka Uholanzi hati iliyoandikwa katika Kiingereza ya kupinga uteuzi wa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen.

Hatua ya chama cha SPD ya kukataa kuunga mkono mgombea kutoka Ujerumani, Ursula von der Leyen, ilisababisha kansela wa Ujerumani Angela Merkel kutoshiriki katika kikao cha Baraza la Ulaya wakati nchi 27 zilikuwa zimemuunga mkono waziri wa wa ulinzi wa Ujerumani.