UINGEREZA-EU-SIASA-UCHUMI

Boris Johnson: Iwapo viongozi wa EU watakataa, Uingereza itajitoa bila makubaliano

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson. REUTERS/Benoit Tessier

Maofisa wa juu wa Umoja wa Ulaya wamekosoa sera ya Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Boris Johnson kuhusu nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake Waziri Mkuu mpaya wa Uingereza Boris kwa wabunge, amesisitiza azma yake ya kumaliza suala tata kuhusu mpaka wa Ireland, kauli ambayo imetupiliwa mbali na kiongozi wa majadiliano wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier.

Boris amezitaka nchi za Ulaya kufikiria upya kuhusu mkataba uliopo sasa, suala ambalo ni wazi Umoja wa Ulaya ulishasema hauko tayari kuubadili.

Waziri mkuu Boris anataka katika siku 88 zilizosalia kabla ya October 31, kuhakikisha anakuwa na mazungumzo mapya na wakuu wa Umoja wa Ulaya kujaribu kupata mkataba anaosema bora zaidi ya ule wa sasa. lakini ameonya kwamba iwapo viongozi wa Umoja wa Ulaya watakataa, Uingereza itajitoa bila makubaliano.