Pata taarifa kuu
POLAND-SIASA

Poland: Spika wa bunge atangaza kujiuzulu

Spika wa Bunge la Polandi Marek Kuchcinski (katikati) akizuru Bunge la Uturuki Oktoba 27, 2016 Ankara.
Spika wa Bunge la Polandi Marek Kuchcinski (katikati) akizuru Bunge la Uturuki Oktoba 27, 2016 Ankara. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Spika wa Bunge nchini Poland, Marek Kuchcinski, ametangaza leo Alhamisi azma yake ya kujiuzulu kwenye wadhifa wake, baada ya kushtumiwa kutumia ndege za serikali kwa safari zake binafsi.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja katika mazingira ya mvutano na kashfa miezi miwili tu kabla ya uchaguzi wa wabunge.

"Kesho nitajiuzulu kwenye wadhifa wa spika wa Bunge," Marek Kuchcinski amewaambia waandishi wa habari, huku akidai kuwa hajavunja sheria kutokana na safari zake nyingi.

Tangazo kwa waandishi wa habari lilitolewa mbele ya kiongozi wa juu katika siasa ya Poland, Jaroslaw Kaczynski, kiongozi wa chama cha Conservative kiliopo madarakani, siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa chama hicho ulidumu masaa kadhaa.

Kwa mujibu wa upinzani na baadhi ya wanahabari, wakinukuu hati kadhaa, Kuchcinski, mwenye umri wa miaka 63, ambaye ni kiongozi namba mbili katika nchi ya Poland kulingana na katiba ya nchi, alitumia Gulfstream, helikopta na ndege za jeshi mara mia kati ya mwezi Machi 2018 na mwezi Mei 2019.

Kulingana na hati hizi, ambazo zilifichuliwa kwa shinikizo kutoka vyombo vya habari na upinzani, Bw. Kuchcinski aliambatana na watu wa familia yake, marafiki zake na baadhi ya wanachama wenzake. Safari nyingi zilifanyika mwishoni mwa wiki kati ya Warsaw na mkoa wa Rzeszow, ambapo anazaliwa na ni mbunge kutoka eneo hilo.

Mapema Jumatatu, Bw. Kuchcinski, mwanasiasa maarufu wa chama tawala cha PiS na mshirika wa karibu wa Jaroslaw Kaczynski, alijizuia kuomba msamaha "kwa wale wote walio ghadhabishwa na safari hizo", na kuongeza kuwa safari nyingi muhimu zilifanyika kutokana na kazi yake ya kisiasa kama Spika wa Bunge.-

Hata hivyo amekiri kwamba wakati fulani mkewe alisafiri kwa ndege na hakuweza kuambatana naye. Ili kulipia gharama ya safari hiyo ya mkewe, Kuchcinski ametangaza kwamba atalipa pesa za Poland Zlotys 28,000 (sawa na Euro 6,500) kwa mfuko unaolenga kuimarisha jeshi, akiwa tayari amelipa zloty 15,000 kwa mashirika ya misaada kwa kulipia gharama aua nauli ya ndege kwa ndugu wa familia yake, kiwango ambacho kinatajwa na wakosoaji wake kuwa hakitoshi.

"Spika wa bunge hajakiuka sheria katika jambo hilo, nataka kusisitiza," amesema Kaczynski leo Alhamisi, ambaye chama chake cha PiS kinapewa nafasi kubwa ya kushinda katiika uchaguzi wa wabunge ambao umepangwa kufanyika Oktoba 13.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.