Pata taarifa kuu
ITALIA-USALAMA-SIASA

Italia yadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuporomoka kwa daraja la Genoa

Daraja la Morandi la Genoa, Agosti 15, 2018.
Daraja la Morandi la Genoa, Agosti 15, 2018. REUTERS/Stefano Rellandini/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Italia inaadhimisha leo Jumatano kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuporomoka kwa daraja la Genoa, ambalo liligharimu miasha ya watu 43 Agosti 14, 2018.

Matangazo ya kibiashara

Siku hii inafika wakati Italia inakabiliwa na mzozo wa kisiasa ambapo Matteo Salvini, kiongozi wa vuguvugu la mrengo wa kulia anataka kuvunja muungano wa vyama unaotawala.

Wahusika wakuu wa mgogoro ulioibuka katikati ya mwei Agosti mwaka huu ambao watakuwa Genoa ni pamoja na Rais Sergio Mattarella, ambaye ndiye aliye na mamlaka ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi, Waziri wa Mambo ya Ndani Salvini ambaye anaomba tangu Agosti 8 kufanyika kwa uchaguzi huo na mshirika wake wa zamani katika serikali Luigi Di Maio, kiongozi wa vuguvugu la M5S, pamoja na Waziri Mkuu Giuseppe Conte na mawaziri kadhaa.

"Ninawaalika raia wote wa Genoa kushiriki katika sherehe hii kwa kuwakumbuka wahanga wa daraja la Morandi na ninaomba wale ambao hawataweza kuhudhuria, wasalie kimya kwa muda wa dakika moja kuwakumbuka ndugu zao, saa 11:36" wakati daraja lilipoanguka, amesema Meya wa mji huo Marco Bucci.

Maadhimisho hayo ni pamoja na misa ya kitakayoongozwa na Askofu Mkuu wa Genoa, Kardinali Angelo Bagnasco, ikifuatwa na hotuba ya meya, waziri mkuu na wawakilishi wa familia za wahanga.

Maadhimisho hayo yatafanyika karibu na eneo ambalo daraja liliporomoka, mita chache na eneo ambapo kumewekwa jiwe la msingi wa daraja jipya, ambapo ujenzi utakamilika msimu ujao wa masika, maafisa wamesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.