Pata taarifa kuu
UFARANSA-URUSI-G7-USHIRIKINAO

Macron kuzungumza na Putin Brégançon kuhusu matatizo yanayoendelea duniani

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, St Petersburg, Mei 24, 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, St Petersburg, Mei 24, 2018. ©REUTERS/Grigory Dukor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kumpokea mwenzake wa Urusi Vladimir Putin katika eneo la Brégançon leo Jumatatu jioni Agosti 19.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa nchi saba zenye nguvu duniani (G7) katika mji wa Biarritz ambapo Urusi haitoshiriki - baada ya kutengwa katika kundi hili tangu kuvamia eneo la Crimea na kulifanya moja ya sehemu yake ya ardhi mnamo 2014 - Rais wa Ufaransa anataka kuzungumza na mwenzake wa Urusi, ambaye anamchukuliwa kama mshirika wake muhimu, maswala makubwa ya kimataifa.

Wawili hao waliafikiana kukutana mnamo mwezi Juni katika mkutano wa nchi 20 zilizostawi kiviwanda.

Mwaka jana, Emmanuel Macron alimpokea Theresa May, na sasa ni zamu ya Vladimir Putin. Rais Putin anatarajiwa kupokelewa kwa heshima huko Brégançon. kulingana na taarifa kutoka ikulu ya Elysee, Brégançon inachukuliwa kama sehemu ya "kazi" ya Rais wa Jamhuri.

Mazungumzo kati ya rais Emmanuel Macron na Vladimir Putin hayatakuwa rahisi, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka ikulu ya Elysee.

Kwenye ajenda ya mazungumzo yao, kuna hususan suala la migogoro nchini Iran, Syria, Ukraine ... Na matatizo yanayoendelea ulimwenguni, hususan mabadiliko ya tabia nchi, usalama, nishati. Masuala mengi yatazungumziwa pia katika mkutano wa G7 ambapo Vladimir Putin hatoshiriki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.