Pata taarifa kuu
ITALIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Meli iliyokuwa ikiabiri wahamiaji yatia nanga Lampedusa

Meli ya shirika la Open Arms kutoka Uhispaniayatia nanga muda mfupi kabla ya saa sita usiku, 20 Agosti 2019 kwenye bandari ya Lampedusa, Sicily.
Meli ya shirika la Open Arms kutoka Uhispaniayatia nanga muda mfupi kabla ya saa sita usiku, 20 Agosti 2019 kwenye bandari ya Lampedusa, Sicily. REUTERS/Guglielmo Mangiapane
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Wahamiaji zaidi ya mia moja waliokolewa katika pwani ya Libya ambao walikuwa wakisafiri na meli ya shirika la Open Arms wamewasili tangu Jumanne usiku, Agosti 20, kwenye kisiwa cha Italia cha Lampedusa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya wakimbizi hao kukwama baharini kwa siku 19 baada ya Waziri wa Mambo ya ndani Matteo Salvini kuwazuia kuingia nchini Italia, na maafisa wamesema walichukizwa kutokana na uamuzi wake.

Wengi wameonekana wakiwa na majeraha na wakitembelea kwa kuchechema baada ya kuondoka katika meli walimokuwemo.

Mwendesha mashtaka wa Agrigento nchini Italia ameamuru meli hiyo ilioabiri wahamiaji ho kutia nanga kwenye bandari ya kisiwa hicho.

Meli hiyo iliingia bandarini saa 5:30 usiku, huku wakaazi zaidi ya hamsini kutoka eneo hilo wakipokea wahamiaji kwa shangwe na nderemo. Wahamiaji walishuka kwa makundi madogo.

Wengi wa wahamiaji wameonekana wakiwa na majeraha na wakitembelea kwa kuchechema baada ya kuondoka katika meli walimokuwemo.
Wengi wa wahamiaji wameonekana wakiwa na majeraha na wakitembelea kwa kuchechema baada ya kuondoka katika meli walimokuwemo. REUTERS/Guglielmo Mangiapane
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.