Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Rais wa Ufaransa ahutubia mabalozi

Rais Macron katika mkutano wa mabalozi Paris Agosti 27, 2019.
Rais Macron katika mkutano wa mabalozi Paris Agosti 27, 2019. Yoan Valat/Pool via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Siku moja baada ya kumalizika kwa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yaliyostawi zaidi kiuchumi duniani (G7), Emmanuel Macron ameongoza mkutano wa jadi wa mabalozi, unaofanyika kila mwaka katika kipindi kama hiki kwenye Ikulu ya Elysee.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ulikuwa fursa kwa rais wa Jamhuri kujadili mwelekeo wa sera yake ya kigeni kwa miezi ijayo.

Rais wa Ufaransa ameanza hotuba yake kwa mabalozi kwa hoja moja: agizo la kimataifa linakabiliwa leo na mabadiliko ya kijiografia, kiuchumi na kiikolojia ambayo yanashuhudiwa katika nchi za Magharibi.

Tabia na mafundisho ambayo diplomasia ya Ufaransa ilitegemea kwa miongo kadhaa havitumiki tena, amesema Emmanuel Macron, ambaye amebaini kwamba haitakiwi tu kuzoea mabadiliko, lakini kujaribu kuunda upya utaratibu wa muongozo mpya wa dunia.

Agizo au muongozo ambao Ulaya inapaswa kutegemea zaidi ikiwa haitaki kupotea, ameonya Rais Emmanuel Macron, ambaye ameongeza mkakati wa diplomasia ya Ufaransa ni sehemu ya mkakati wa Ulaya.

Jumuiya ya Ulaya inapaswa kwa gharama zote, kuimarisha uhuru wake wa kiuchumi na kibiashara, kijeshi au kimkakati, Rais Emmanuel Macron ameomba.

Paris inaweza na inapaswa pia ichukue jukumu la nguvu ya usawa, amesema Macron

Baada ya kumpokea wiki iliyopita Vladimir Putin huko Brégançon, Bwana Macron amesema anaamini kuhusu ulazima wa Umoja wa Ulaya kuwa na uhusiano mpya na Urusi.

Lakini pia kubaini umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na China, ambayo Rais Macron amesifu juhudi hizo, haswa kuhusu ikolojia.

Uhuru pia unaanzia kwenye ulinzi wa mipaka ya Umoja wa Ulaya. Katika hatua hii, hakuna tangazo jipya, lakini uthibitisho wa mkakati wa uhamiaji ambao tayari umewekwa. Hiyo ni kusema kuzuia watu kutoroka nchi zao, kuharakisha zoezi la kuwarudisha nyumbani wahamiaji na kufungua njia halali kwa watu wanaostahiki kupewa ukimbizi.

LakiniEmmanuel Macron amesema haoni mahali pa Ufaransa katika mkakati wa Umoja wa Ulaya; Ufaransa inaweza na inapaswa pia kuchukuwa jukumu la nguvu ya usawa, amehakikisha rais Macron. Kwa upande wake amesema, diplomasia ya Ufaransa inaweza kumudu uhuru na kubadilika kuwa muhimu wakati wa migogoro ya kimataifa.

Rais Macron amezungumzia suala la Irani, ambalo Paris imeweza kupunguza joto katika mgogoro huo, hata kama Emmanuel Macron amekiri kwamba matokeo yake ya kwanza kwenye mkutano wa G7 bado ni dhaifu sana.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.