UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Raia wa Uingereza waghadhabishwa na hatua ya kusitishwa vikao vya bunge

Waziri Mkuu wa Uingereza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin Agosti 21, 2019.
Waziri Mkuu wa Uingereza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin Agosti 21, 2019. Tobias SCHWARZ / AFP

Baada ya Malkia kukubali ombi la Waziri Mkuu mpya nchini Uingereza Boris Johnson, kusitisha vikao vya bunge, hali ya sintofahamu imeibuka kati ya wanasiasa.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kusitisha vikao vya bunge umesababisha ghadhabu kutoka kwa wabunge na wapinzani wanaopinga kuidhinishwa Brexit bila mpangilio.

Bunge la Uingereza litasitisha vikao vyake hadi Oktoba 14. Sawa na siku kumi na tano kabla ya tarehe iliyopangwa ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit).

Upinzani umelaani hatua hiyo na kuita kuwa ni ya kiimya, huku ukimshtumu Boris Johnson kwamba lengo lake ni kuwanyamazisha wabunge ili afikie ndoto yake ya kutaka uingereza ijitoe katika Umoja wa Ulaya bila mkataba.

Hatua hiyo ilichangia kuzuka maandamano kote nchini, kesi iliowasilishwa dhidi ya hatua hiyo na waraka uliosainiwa na zaidi ya watu milioni moja kupinga hatua hiyo.

"Boris Johnson alisema atakuwa mfalme wa dunia. Lakini kauli yake hiyo sio. Yeye ni Waziri Mkuu, na anapaswa kuchukua hatua kwa maslahi ya taifa. Badala yake, anajaribu kutaka Uingereza ijitoe katika Umoja wa Ulaya kwa nguvu bila mkataba kupitia kupitia wananchi wa Uingereza. Hatu aliochukuwa ni kinyme na demokrasia, kwanza waziri mkuu mwenyewe hajachaguliwa na raia, " amesema Jo Swinson, mmoja wa wabunge wa upinzani.