Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Johnson kuwasilisha muswada wa kuitisha uchaguzi wa mapema

Waziri Mkuu Boris Johnson apata pigo kwa kura ya kuzuia Brexit ya bila makubaliano.
Waziri Mkuu Boris Johnson apata pigo kwa kura ya kuzuia Brexit ya bila makubaliano. PRU / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Waziri Mkuu wa Uingereza amesema, atawasilisha muswada bungeni, kuomba Uchaguzi Mkuu wa mapema kufanyika mwezi ujao. Ili aweze kuitisha uchaguzi wa mapema, muswada huo utapaswa kupitishwa na theluthi mbili ya wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja, baada ya upande wa serikali usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumtatu, kushindwa kupitsiha mswada ambao ungeinfanya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya mkataba ifikapo mwisho wa mwezi ujao.

Serikali ya waziri mkuu imepoteza wingi wa viti bungeni, baada ya mbunge wa Conservative Phillip Lee kuhama upande wa chama hicho na kuketi upande wa Liberal Democrats, wakati waziri mkuu alipokuwa akizungumza katika baraza la chini la bunge la Uingereza.

Wabunge 21 wa chama cha Boris Johnson waliugana na wabunge wa upinzani kupinga mkataba huo, wanataka Uingereza ijiondoe kwenye Umoja wa Ulaya na mkataba.

Wakati huo huo msemaji katika ofisi ya waziri mkuu amesema wabunge wote 21 waasi wa Conservative walioipinga serikali ya Johnson watafukuzwa ndani ya chama

Wabunge wamepiga kura 328 dhidi ya 301, kuunga mkono juhudi za kuzuia mpango wa taifa hilo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

Hatua hiyo sasa inapisha njia kwa wabunge kupitisha sheria baadae leo Jumatano, ambayo itamshinikiza Waziri mkuu Boris Johnson kuuomba Umoja wa Ulaya kuchelewesha tena Brexit, jambo ambalo amesema hatolifanya chini ya mazingira yoyote.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.