Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHUMI-SIASA

Spika wa Bunge la Ufaransa Richard Ferrand afunguliwa mashitaka

Richard Ferrand katika kikao cha Bunge Septemba 2018, wakati akichukua hatamu ya uongozi wa bunge.
Richard Ferrand katika kikao cha Bunge Septemba 2018, wakati akichukua hatamu ya uongozi wa bunge. REUTERS/Charles Platiau/FIle Photo
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Spika wa Bunge la Ufaransa, Richard Ferrand, amefunguliwa mashitaka usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii katika mji wa Lille kwa kuchukua haki haramu katika kesi ya Mutuelles de Bretagne. Richard Ferrand amekana tuhuma hizo dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya "kuhojiwa wakati akisikilizwa kwa mara ya kwanza" kwa muda wa saa 15 katika Mahakama ya mjini Lille, ambapo kesi hiyo ilifunguliwa mwaka mmoja uliopita, "majaji watatu wa mahakama ya mwanzo waliokabidhiwa kesi hiyo, wameamua kumfungulia mashitaka Richard Ferrand kwa kuchukua haki haramu, "ofisi ya Mashitaka ya Lille imeliambia shirika la Habari la AFP Jumatano usiku.

Kesi ya Mutuelles de Bretagne ilianza mwaka 2011 baada tu ya kuteuliwa Waziri wa Ushirikiano wa utawala, na baadae alitajwa na gazeti la Le Canard ambapo lilibaini kwamba mnamo mwaka 2011 Mutuelles de Bretagne, ambalo shirika ambalo alikuwa anaongoza wakati huo, liliamua kukodisha majengo ya biashara ya rafiki yake.

Richard Ferrand amebaini kwamba sheria za zabuni zilifuatishwa kwa kukodisha majengo hayo. Mkasa huu ulisababisha Richard Ferrand, mshirika wa karibu wa sasa wa Emmanuel Macron kujiuzulu serikalini mnamo mwezi Juni 2017.

Richard Ferrand ni Spika wa Bunge tangu mwezi Septemba 2018, na ni kiongozi wa nne nchini Ufaransa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.