Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Uchaguzi wa mapema Uingereza: Johnson aendelea kutafuta uungwaji mkono

Umoja wa Ulaya umekubali kuchelewesha kwa muda wa miezi mitatu Uingereza kujitoa kutoka Umoja huo hadi Januari 31.
Umoja wa Ulaya umekubali kuchelewesha kwa muda wa miezi mitatu Uingereza kujitoa kutoka Umoja huo hadi Januari 31. Kenzo Tribouillard/Reuters via pool
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajia kujaribu tena leo Jumanne kupata uungwaji mkono kuhusu uchaguzi wa mapema mwezi Desemba ili kuokoa mchakato wa Brexit, ambao umeahirishwa kwa mara ya tatu.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya nakala inayoitisha uchaguzi wa wabunge Desemba 12 kukataliwa Jumatatu na Baraza la Wawakilishi, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kwamba anaandaa kura mpya kuhusu kufanyika kwa uchaguzi wa mapema. Anatumai kwamba kupitia uchaguzi huo atakuwa na wabunge wengi ambao watamuwezesha kutimiza ahadi yake ya kutekeleza mchakato wa Brexit, miaka mitatu na nusu baada ya kura ya maoni ya mwaka 2016.

Wakati Boris Johnson aliahidi kuitoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya "kwa njia yoyote ile" hadi Oktoba 31, akisema "afadhali afe chini ya shimo" badala ya kuomba kuahirishwa kwa mchakato huo, Umoja wa Ulaya umekubali Jumatatu wiki hii kuchelewesha kwa muda wa miezi mitatu Uingereza kujitoa kutoka Umoja huo hadi Januari 31.

Kiasi siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya hapo Oktoba 31, mchakato wa Brexit bado haujulikani mwelekeo wake wakati wanasiasa wa Uingereza hawako karibu ya kufikia muafaka juu ya vipi, lini na hata iwapo hatua ya kuachana na Umoja wa Ulaya itawezekana. Mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya yamefikia makubaliano Jumatatu wiki hii kuchelewesha Brexit hadi Januari 31, pamoja na uwezekano wa Uingereza kujitoa mapema iwapo bunge la Uingereza litaidhinisha makubaliano ya kujitoa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.