Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-KAMPENI-USHIRIKIANO-SIASA

Boris Johnson na mpinzani wake mkuu Jeremy Corbyn wanadi sera zao

Kambi ya wanaopinga Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya wakiandamana mbele ya makao makuu ya bunge London, Septemba 4, 2019.
Kambi ya wanaopinga Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya wakiandamana mbele ya makao makuu ya bunge London, Septemba 4, 2019. REUTERS/Henry Nicholls

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amezindua rasmi kampeni za chama chake cha Conservative katika mji ambao kihistoria, ni ngome ya chama kikuu cha upinzani cha Labor huku akiahidi kuhakikisha anakamilisha mchakato wa Brexit ikiwa atapata ushindi.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea na wafuasi wa chama hicho, Boris amewataka wampe kura zitakazowezesha kupata wabunge wengi ili akamilishe mchakato wa nchi hiyo kujitoa Umoja wa Ulaya.

Kwa upande wake kinara wa upinzani kutoka chama cha Labor, Jeremy Corbyn, amesema ikiwa atachaguliwa atahakikisha analeta mabadiliko ya kweli ambayo chama cha Conservatives kimeshindwa.

Vyama kadhaa pia vilizindua kampeni zao baada ya Waziri Mkuu Boris kuwasilisha barua kwa malkia Elizabeth kumtaarifu kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Desemba 12.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.