UINGEREZA-NATO-USALAMA

NATO yajaribu kuweka mambo sawa baada ya tofauti zilizojitokeza

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na rais wa Marekani Donald Trump pembezoni mwa mkutano huo, ameonekana kutofurahishwa kuhusu vita dhidi ya makundi ya kigaidi kama Islamic State.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na rais wa Marekani Donald Trump pembezoni mwa mkutano huo, ameonekana kutofurahishwa kuhusu vita dhidi ya makundi ya kigaidi kama Islamic State. Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Viongozi kutoka mataifa ya Magharibi yanayounda jeshi la pamoja la kujilinda NATO, wanatarajiwa kujaribu kuzungumza kwa sauti mmoja wanapokutana leo Jumatano jijini London nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Kuelekea katika kikao hiki muhimu, viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya NATO, wameonekana kutofautiana kuhusu majukumu yao katika jeshi hilo hasa kuhusu operesheni za kiusalama dhidi ya magaidi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na rais wa Marekani Donald Trump pembezoni mwa mkutano huo, ameonekana kutofurahishwa kuhusu vita dhidi ya makundi ya kigaidi kama Islamic State.

Jumanne wiki hii Rais wa Marekani alimkosoa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kusema Nato ni 'ubongo uliokufa'.

Bwana Macron alielezea muungano huo kama "ubongo uliokufa", akisisitiza kile anachokiona kama kutokuwa na utashi wa mdhamini mkuu, Marekani.