Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA-MACRON-MALIPO

Rais Macron asisitiza mageuzi ya malipo ya uzeeni

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Yves Herman

Rais wa Ufaransa Emmanue Macron, amesema lengo lake ni kuimarisha mfumo wa malipo ya Pensheni na kusisitiza kuwa hana nia ya kuachana na mabadiliko aliyoanzisha ambayo yanapingwa na vyama vya wafanyikazi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Ikulu jijini Paris, imemnukuu afisa wa juu serikalini amesema kuwa, rais Macron hana mpango wa kuachana na mchakato wa mabadiliko aliyoanzisha, na badala yake ataifanyia marekebisho ili uwe bora zaidi.

Suala tata ambalo limezua maandamno makubwa ni kuwa, wafanyikazi watasubiri hadi umri wa miaka 64 ili kupata malipo yote ya uzeeni baada ya kustaafu, mabadiliko ambayo yanafanyika baada ya miaka zaiid ya 40.

Maandamano yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa wiki mbili sasa, na kusababisha kukwama kwa shughuli kama usafiri wa umma na kuwatatiza raia wa nchi hiyo.

Jana kulikuwa na maandamano ya maelfu ya watu, kupinga mageuzi hayo, huku kila upande ukisimamia maamuzi yake wakati huu serikali ikisema iko tayari kwa mazungumzo ili kupata suluhu.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.