UFARANSA-PENSHENI-JAMII

Salamu 2020 : Emmanuel Macron aapa kuendelea mabadiliko ya sheria ya pensheni hadi tamati

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron metoa salaamu za Mwaka Mpya 2020 kwa Wafaransa, Jumanne hii, Desemba 31, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron metoa salaamu za Mwaka Mpya 2020 kwa Wafaransa, Jumanne hii, Desemba 31, 2019. www.elysee.fr/

Akiwa katika mapunziko tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya mabadiliko ya sheria ya pensheni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwahutubia wananchi wake amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuendelea na mpango huo hadi tamati.

Matangazo ya kibiashara

Rais Macron ameitaka serikali ya waziri Mkuu Edouard Philippe kuharakisha kupatikana kwa suluhu ya mzozo huo ambao umeidhofisha pakubwa serikali yake.

Rais Emmanuel Macron amejaribu kutuliza mzozo huo unaotokana na mabadiliko ya sheria ya pensheni ambao umeendelea kukuwa na kuonekana kuwa mzozo mkubwa kuwahi kutokea nchini Ufaransa.

Rais Macron ametowa wito pia wa umoja wa kitaifa.

Emmanuel Macron amesema hivi karibuni atachukuwa maamuzi mapya dhidi ya wale wote wanaotaka kuvunja Umoja.