UFARANSA-SARKOZY-HAKI

Rais wa zamani wa Ufaransa kufikishwa mahakamani mwezi Oktoba

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akabiliwa na tuhuma za ufisadi. Kenzo TRIBOUILLARD / AFP

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atafikishwa Mahakamani mwezi Oktoba kujibu mashtaka ya ufisadi. Sarkozy anadaiwa kujaribu kupokea taarifa muhimu kutoka kwa Jaji kuhusu uchunguzi dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kushatkiwa ndani ya miaka 60 kwa tuhma za ufisadi katika taifa hilo la bara Ulaya.

Nicolas Sarkozy anakabiliwa na tuhuma kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Mwaka 2013, Ufaransa ilianzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba kampeni ya Sarkozy ilipokea mchango kutoka kwa hazina ya pesa haramu za Gaddafi.

Bw Sarkozy amekanusha tuhuma hizo.

Novemba 2016, Ziad Takieddine aliambia kituo cha habari cha Mediapart kuwa kati ya 2006-2007, alikabidhi mikoba mitatu iliyojaa noti za euro 200 na 500 kwa Bw Sarkozy na mkuu wa watumishi wake Claude Guéant.

Bw Takieddine aanadai pesa hizo zilitoka kwa Gaddafi nazilikuwa takriban Dola milioni 6.2 sawa na Euro milioni 5.