UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Ushirikiano wa baada ya Brexit: Mazungumzo ya awali chini ya mvutano kati ya London na EU yaanza

Waziri Mkuu Boris Johnson (kushoto) na kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo kuhusu Brexit, Michel Barnier, Oktoba 17, 2019 huko Brussels.
Waziri Mkuu Boris Johnson (kushoto) na kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo kuhusu Brexit, Michel Barnier, Oktoba 17, 2019 huko Brussels. © AFP

Mazungumzo kuhusu uhusiano wa baada ya Brexit kati ya London na Umoja wa Ulaya yanaanza leo Jumatatu huko Brussels katika hali ya mvutano na chini ya shinikizo la kalenda, hali ambayo inakatisha imani kwa kufikia makubaliano.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo Michel Barnier na mwenzake wa Uingereza David Frost wanakutana leo mchana kwa mazungumzo ya saa moja. Halafu duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya timu zao imepangwa kufanyika hadi Alhamisi wiki hii.

Baada ya wiki iliyopita kuchapishwa maswala ambayo yatajadiliwa na kambi hizo mbili, ambapo kila upande ulionyesha msimamo wake, na hivyo kuonyesha mgawanyiko mkubwa, suala ni kujuwa iwapo watafikia makubaliano.

Iwapo watashindwa kuafikiana, uchumi unaweza kuwa hatarini, kwa Uingereza lakini pia kwa bara la Ulaya.

Tathmini ya kwanza ya mazungumzo ilipangwa kuanza mwezi Juni, Hata hivyo serikali ya Boris Johnson imetoa tarehe ya mwisho na Alhamisi iliyopita ilitishia kujiondoa kwenye mazungumzo hayo wakati wa kiangazi ikiwa watashindwa kuafikiana.