UTURUKI-EU-UGIRIKI-WAHAMIAJI

Erdogan aitaka Ugiriki kufungua mipaka yake kuruhusu wahamiaji kuingia Ulaya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anafanya ziara ya kiserikali Jumatatu hii katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, kwa mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya wahamiaji.

Viosi vya usalama vyatumia mizinga ya maji kwa kusambaratisha umati wa wahamiaji waliokusanyika kwenye mpaka wa Uturuki na nchi hiyo karibu na mpaka wa Pazarkule, Uturuki, Machi 7, 2020.
Viosi vya usalama vyatumia mizinga ya maji kwa kusambaratisha umati wa wahamiaji waliokusanyika kwenye mpaka wa Uturuki na nchi hiyo karibu na mpaka wa Pazarkule, Uturuki, Machi 7, 2020. REUTERS/Huseyin Aldemir
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Rais huyo wa Uturuki amesema ana imani atapata matokeo tofauti baada ya mazungumzo ya Jumatatu wiki hii.

Jumapili Machi 8, 2020, rais wa Uturuki aliitaka Ugiriki "kufungua milango yake" kwa wahamiaji - ambao Ankara ilitangaza mwishoni mwa mwezi wa Februari kwamba ilifungua mipaka yake - na kuwaruhusu waingie katika barani Ulaya. Rais Erdogan anaonekana anapanga kupata mkataba uliorekebishwa Machi 2016 kuhusu wahamiaji.

Recep Tayyip Erdogan alibaini kwamba haombi Ugiriki kuwapkea wahamiaji. "Watu hawa hawatabakia katika nchi yako. Watapita tu kwenda nchi zingine za Ulaya, "alisema rais wa Uturuki. Na kuongeza: "Jikomboe kutoka kwa mzigo huu wa wahamiaji. "

Akizungumza mjini Istanbul, Erdogan amesema Uturuki haijaungwa mkono katika suala la wakimbizi na Jumuiya ya kimataifa kama ilivyokuwa ikitarajia.

Uturuki imekuwa ikikosoa kile inachokielezea kuwa ni ugavi wa mzigo wa wakimbizi usio na usawa, wakati nchi hiyo ikiwa na takribani wahamiaji milioni nne wanaoishi nchini humo, wengi wao wakiwa kutoka Syria.