ULAYA-CORONA-AFYA

Uamuzi wa kulegeza masharti ya watu kukaa nyumbani wakaribishwa Ulaya

Kazi zimeanza tena Mei 4 katika kampuni kadhaa nchini Italia, kama hapa kwenye kiwanda cha NTN-ICSA huko San Benigno Kanavese.
Kazi zimeanza tena Mei 4 katika kampuni kadhaa nchini Italia, kama hapa kwenye kiwanda cha NTN-ICSA huko San Benigno Kanavese. REUTERS/Massimo Pinca

Ulaya imeanza ukurasa mpya wa kulegeza masharti ya kutotembea baada ya watu wake kujifungua ndani kwa hofu ya kuambukizwa ugonjwa hatari wa Covid-19 ulioanzia katikati mwa China, katika jiji la Wuhan mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Ugojnwa wa Covid-19 umeua watu zaidi ya 250,000 duniani.

Kwa matumaini ya kuongeza fedha kufadhili utaftaji wa chanjo na matibabu, Umoja wa Ulaya umeandaa mkutano wa kimataifa wa wafadhili huko Brussels nchini Ubelgiji Jumatatu wiki hii, na kuungwa mkono na viongozi wakuu wa Ulaya lakini bila Marekani.

Italia, taifa la pili baada ya Marekani kwa kuwa na vifo vingi vya wagonjwa wa Covid-19, limeanza rasmi shughuli za uzalishaji mali siku ya Jumatatu (4 Mei) kwa kufunguwa viwanda na maeneo ya ujenzi.

Uchumi wa Italia, ambao ni wa tatu kwa ukubwa katika Ukanda wa Euro, unatazamiwa kusinyaa katika kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu Mfadhaiko wa Kiuchumi wa Kilimwengu wa miaka ya 1930.

Hayo yanajiri wakati rais wa Marekani Donald Trump ameongeza mashambulizi yake dhidi ya China, akiituhumu kuwa chanzo cha virusi ambavyoo anasema vilianzia kwenye maabara moja mjini Wuhan.

China imefutilia mbali madai hayo.