UJERUMANI-CORONA-AFYA

Ugonjwa wa Covid-19 wauawa watu zaidi 43 nchini Ujerumani

Tangu Jumatatu, Aprili 27, Serikali ya Ujerumani imewataka raia wake kuvaa barakoa, hasa katika sekta ya uchukuzi na karibu kila mahali katika maduka. Hapa ni eneo la Bad Badnef, karibu na Bonn.
Tangu Jumatatu, Aprili 27, Serikali ya Ujerumani imewataka raia wake kuvaa barakoa, hasa katika sekta ya uchukuzi na karibu kila mahali katika maduka. Hapa ni eneo la Bad Badnef, karibu na Bonn. REUTERS/Wolfgang Rattay

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa nchini Ujerumani imeongezeka hadi 163,175, na ugonjwa huo sasa umesababisha vifo vya watu 6,692 nchini humo, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatatu hii Mei 4 na Chuo Kikuu cha Marekani cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Hii inaonesha kuwa visa vipya 679 vya maambukizi na vifo vipya 43 ndani ya masaa ishirini na nne, kulingana na ripoti iliyoripotiwa na RKI.

Hivi karibuni Ujerumani ilianza majaribio ya chanjo ya kwanza dhidi ya virusi vya Corona, iliyotengenezwa nchini humu. Hiyo ni chanjo ya nne ya aina hiyo duniani kupata ridhaa ya kuanza kujaribiwa kwa binadamu.

Inaaminika kuwa kirusi hicho kilianzia katika soko la nyama za wanyama pori katika mji wa Wuhan nchini China kabla ya kusambaa katika maeneo karibu yote ya dunia.

Kampuni nyingi ulimwenguni zinashindana katika utafiti wa kuunda chanjo dhidi ya virusi vya corona ambavyo hadi sasa vimewaambukiza watu zaidi ya milioni 3.5 kote duniani, ukiwauwa zaidi ya 200,000.

Mapema mwakahuu Umoja wa Mataifa uliitahadharisha dunia kuwa nchi maskini ambazo tangu siku za nyuma zilisumbuliwa na uhaba wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi, yumkini athari za janga la virusi vya corona zitaziacha katika hali mbaya zaidi.