UJERUMANI-CORONA-AFYA

Michuano ya soka ya ligi kuu kuanza tena Mei nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Aprili 15, 2020 alipokuwa akitangaza hatua za serikali katika kupambana na janga la Corona.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Aprili 15, 2020 alipokuwa akitangaza hatua za serikali katika kupambana na janga la Corona. AFP/Bernd Von Jutrczenka/Pool

Ujerumani inaapanga kuruhusu michuano ya soka ya ligi kuu kuanza tena mnamo mwezi Mei, baada ya kusitishwa kutokana na janga la Corona, kulingana na rasimu ya makubaliano kati ya Angela Merkel na marais wa majimbo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Kuanza kwa mechi za daraja la kwanza na la pili, ili "kupunguza athari kwa uchumi", "imekubalika" kuanzia kwa tarehe ya mwezi Mei ambayo itatangazwa katika mkutano kwa njia ya simu Jumatano hii, Mei 6, kulingana na hati hiyo, wakati vyombo vya habari vya Ujerumani vinaripoti kuwa michuano inaweza kuanza Mei 21.

Michezo kwa wasio wachezaji na watoto pia itafunguliwa tena.

Chanzo kimoja kimesema kwamba mamlaka pia wana nia ya "kufunguwa tena shule za chekechea kusaidia wazazi wengi wanaofanya kazi.

Mamlaka katika majimbo hayo zinatarajiwa kutoa idhni ya kufungua tena maduka katika majimbo yote ya Ujerumani, labda kuanzia Mei 11, vyanzo hivyo vimesema. Biashara ndogo ndogo tayari zimeruhusiwa kufunguliwa tena kwa masharti ya kuheshimu hatua za kutokaribiana.

jerumani ilifikia hatua mpya Jumatatu wiki hii ya kuanza kulegeza vizuizi ikiwa ni pamoja na kufungua tena majumba ya makumbusho na sehemu za ibada na viwanda kadhaa vya magari, lakini wanasiasa wamegawanyika kuhusu hatua hiyo.