UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Maambukizi yafikia zaidi ya watu 166,000 Ujerumani

Ujerumani inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19 (Corona).
Ujerumani inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19 (Corona). AFP/Torsten Silz

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyothibitishwa nchini Ujerumani imeongezeka hadi 166,091, na ugonjwa huo sasa umesababisha vifo vya watu 7,119 nchini humo, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na Chuo Kikuu cha Marekani cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Hii inaonesha visa vipya 1,294 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 123 ndani ya saa ishirini na nne, kulingana na ripoti ya RKI.

Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 umeuwa watu zaidi ya 255,000 ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 70,000 nchini Marekani, ambayo ni nchi iliyoathiriwa zaidi na mgogoro huu wa kiafya.

Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia waandishi habari mjini Washington kuwa ugonjwa wa Covid-19 umeiathrii Marekani  kwa kiwango kikubwa kuliko mashambulizi ya mabomu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pearl Harbor ya mwaka 1941 au tukio la kigaidi la Septemba 11.

Jumuiya ya wanasayansi wanakubaliana kwamba virusi vya Corona, ambavyo vilianzia katika mji wa China wa Wuhan mwishoni mwa mwaka jana, vilitokea katika soko wanakouza wanyama wa porini na kisha kuenea kwa binadamu.

Tayari nchi kadhaa duniani zimeanza kulegeza masharti yaliyowekwa kudhibiti ugonjwa hatari wa Corona.

Wadadisi wanasema huenda hatua hizi ndizo zikazidisha ugonjwa huo kushika kasi zaidi.