UHISPANIA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Madrid kufungua tena mipaka yake kwa watalii mwishoni mwa mwezi Juni

Polisi ikiwapa abiria marakoa kwenye vituo vya treni za mwendo kasi huko Madrid, Aprili 13, 2020.
Polisi ikiwapa abiria marakoa kwenye vituo vya treni za mwendo kasi huko Madrid, Aprili 13, 2020. REUTERS/Susana Vera

Uhispania inatarajia kufungua tena mipaka yake kwa watalii mwishoni mwa Juni kwa matumaini ya kufufua tena sekta hiyo shughuli zake zilikuwa zimekwama kutokana na vizuizi vilivyowekwa na serikali kwa kudhbiti Corona.

Matangazo ya kibiashara

Uhispania imerikodi visa 231,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 27,650 nchini humo. Wagonjwa 150,000 wamepona ugonjwa huo.

"Mara tu raia wa Uhispania kuruhusiwa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine, raia wa kigeni watarejea tena Uhispania," Jose Luis Abalos, waziri wa utalii wa Uhispania, amesema kwenye televisheni ya TVE.

"Kuanzia mwisho wa mwezi Juni, tutaanzisha tena shughuli za utalii, nina imani na hilo," ameongeza.

Uhispania, nchi ambayo utalii unafanya asilimia 12 ya Pato la Taifa, kufungua tena mipaka yake na kurudi kwa watalii ni muhimu kwa uchumi ambao, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Uhispania, unaweza unaweza kuongezeka kwa asilimia 12,4 mwaka huu.