UHISPANIA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Uhispania kufungua tena mipaka yake ya ardhini na Ufaransa na Ureno

Uhispania imerikodi visa 240,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 27,128 nchini humo.
Uhispania imerikodi visa 240,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 27,128 nchini humo. Community of Madrid/Handout via REUTERS

Uhispania, kupitia waziri wake wa Utalii Reyes Maroto, imetangaza kwamba itafungua upya mipaka yake ya ardhini na Ufaransa pamoja na Ureno Juni 22 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa upande wa Ufaransa na Ureno, nilitaka kuthibitisha kwamba kuanzia Juni 22 vizuizi katika mpaka ya ardhini vitaondolewa," Reyes Maroto amesema wakati wa mkutano na vyombo vya kimataifa, akibaini kwamba "karantini (...) zitaondolewa ".

Hivi karibuni Uhispania ilitangaza kwamba inatarajia kufungua tena mipaka yake kwa watalii mwishoni mwa mwezi Juni kwa matumaini ya sekta hiyo kufufua tena shughuli zake zilizokuwa zimekwama kutokana na vizuizi vilivyowekwa na serikali kwa kudhbiti Corona.

Uhispania imerikodi visa 240,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 27,128 nchini humo. Wagonjwa 150,000 wamepona ugonjwa huo.

Uhispania, nchi ambayo utalii unafanya asilimia 12 ya Pato la Taifa, kufungua tena mipaka yake na kurudi kwa watalii ni muhimu kwa uchumi ambao, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Uhispania, unaweza kuongezeka kwa asilimia 12,4 mwaka huu.