Coronavirus: Zaidi ya visa 183,000 vya maambukizi vyathibitishwa Ujerumani
Imechapishwa:
Idadi ya visa vya mambukizi virusi vya Corona vilivyothibitishwa nchini Ujerumani imepanda hadi 183,271, baada ya visa vipya 394 kuthibitishwa ndani ya kipindi cha saa 24, kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Robert Koch (RKI).
Vifo vya vipya ishirini na sita vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo 8,736 tangu kuzuka kwa janga la Covid nchini Ujerumani, Chuo Kikuu cha Robert Koch kimebaini.
Hata hivyo wagonjwa 168,000 wamepona ugonjwa wa Covid-19.
Wakati huo huo nchini Ufaransa janga la Covid-19 limedhibitiwa, kulingana na wataalam.
Mlipuko wa Covid-19 kwa sasa "unadhibitiwa" nchini Ufaransa, amesema Mwenyekiti wa bodi ya Sayansi, Profesa Jean-François Delfraissy.
Umma"Virusi vinaendelea kusambaa kwa kasi ndogo, hasa katika baadhi ya mikoa", profesa Jean-Paul Delfraissy amesema kwenye radio ya France Inter.