UFARANSA-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron ziarani London kwa maadhimisho ya miaka 80 ya hotuba ya Juni 18

Emmanuel Macron anafanya ziara jijini London, nchini Uingereza Alhamisi wiki hii kwa maadhimisho ya miaka 80 ya hotuba ya Jenerali de Gaulle, afisa wa juu wa jeshi la wa Ufaransa aliyotoa Juni 18 ili kuendelea na vita dhidi ya utawala wa Kinazi nchini Ujerumani.

Emmanuel Macron anafanya ziara jijini London, nchini Uingereza Alhamisi wiki hii hii kwa maadhimisho ya miaka 80 ya hotuba ya Jenerali, aliyoitoa Juni 18 katikavita dhidi ya utawala wa Kinazi Ujerumani. de Gaulle
Emmanuel Macron anafanya ziara jijini London, nchini Uingereza Alhamisi wiki hii hii kwa maadhimisho ya miaka 80 ya hotuba ya Jenerali, aliyoitoa Juni 18 katikavita dhidi ya utawala wa Kinazi Ujerumani. de Gaulle Ludovic Marin/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ni ishara muhimu kwa mataifa hayo mawili, na ni zaiara ya kwanza kwa rais wa Ufransa tangu mwishoni mwa mwezi Februari kwa sababu ya janga la Covid-19.

Emmanuel Macron na ujumbe wake hata hivyo wataepuka masharti ya kizuizini yaliyowekwa kwa wasafiri wanaoingia nchini Uingereza, kulingana na hatua maalumu iliyochukuliwa na serikali ya Uingereza kwa mgeni huyo wa heshima kutoka Ufaransa.

Mfalme wa Wales na mkewe Camilla ndio watamkaribisha rais wa Ufaransa katika makazi yao ya London huko Clarence House. F

Emmanuel Macron atamkabidhi mwanamfalme Charles kijiti cha heshima kama zawadi anayoitoa kwa mji wa London, ambao ulitoa hifadhi kwa taifa la Ufaransa wakati huo baada ya utawala wa kinazi kuvamia nchi ya ufaransa. Meya wa mji wa London Sadiq Khanatahudhuria sherehe hiyo.

Rais Macron atakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika ofisi yake ya Downing Street. Katika hafla hii Waziri Mkuu wa Uingereza atakabidhi zawadi ya MBE, kwa askari wanne ambao bado wako hai, walioshiriki katika vita vya Ukombozi na atamkabidi rais Emmanuel Macron hati zinazohusiana na kumbukumbu ya Jenerali de Gaulle na Winston Churchill.