EU-CORONA-UCHUMI

Viongozi wa EU kujadili mpango wa kusaidia uchumi wa baada ya Corona

Kikao kipya cha Baraza ya Umoja wa Ulaya kitafanyika Ijumaa 19 Juni kupitia video. Hapa, Rais wa Baraza la Umoja Ulaya, Charles Michel, huko Brussels, Juni 18, 2020.
Kikao kipya cha Baraza ya Umoja wa Ulaya kitafanyika Ijumaa 19 Juni kupitia video. Hapa, Rais wa Baraza la Umoja Ulaya, Charles Michel, huko Brussels, Juni 18, 2020. Francisco Seco/Pool via REUTERS

Baraza la Umoja wa Ulaya linakutana leo Ijumaa kupitia video kuchukua hatua muhimu katika mpango wa kuokoa uchumi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya uliosambaratishwa na mripuko wa virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo wa Euro Bilioni 500 ulipendekezwa na Tume ya Umoja wa Ulaya. Makubaliano yanatarajiwa kufikiwa mnamo mwezi Julai: Ufaransa na Ujerumani zimerejelea tena kauli zao saa chache zilizopita, hii itawezesha pesa kufika kwenye hazina za nchi zilizohusika ndani ya kipindi cha miezi sita.

Rais wa Tume ya Umoja aw Ulaya, Ursula von der Leyen, amependekeza uanzishwe mfuko wa uokozi wenye thamani ya euro bilioni 750.

Hata hivyo mataifa wanachama yamegawanyika vibaya juu ya mpango huo. Uholanzi, Sweden, Denmark na Austria, zinaupinga mpango huo, hali inayotishia kutofanikiwa kwake.

Lakini Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uhispania, ambayo yote ni mataifa yaliyokumbwa vibaya na virusi vya korona, yanaunga mkono kuanzishwa kwa mfuko huo.