UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Johnson afutilia mbali shutma kuhusu kutowajibika kwake kama mlipuko wa pili utatokea

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. REUTERS/Lisi Niesner

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametupilia mbali shutma kwamba serikali ya Uingereza haiko tayari kukabiliana na mlipuko wa pili wa janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Wakati Uingereza inajiandaa kuongeza kasi kwa kulegeza masharti dhidi ya Corona, baraza la mawaziri limejadili kuhusu mpango wa kurejesha tena marufuku mapya kwa raia wa ndani ya nchi hiyo ikiwa kutatokea ongezeko la maambukizi mapya. Pia Application mpya inapaswa kutumiwa kuonya watu waliotangamana na watu walioambukizwa virusi vya Corona.

Keir Starmer, kiongozi mpya wa Chama cha Labour, amebaini, wakati wa kikao cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni, kwamba serikali haitakuwa tayari kwa hoja hizi mbili wakati masharti mapya yatakapoanza kutumika, Julai 4 nchini Uingereza.

"Tuna mfumo mzuri sana wa kukomesha maambukizi mapya ambao utadhibiti janga hili," amebaini Boris Johnson.

"Sitakubali kuwa hii itafanya virusi kutoweka (...) Lazima tukae macho na halmashauri za mitaa zitasaidiwa katika kukamilisha kazi hii muhimu inayohusika na kutekeleza masharti ya kudhibiti maambukizi", ameongeza.